|
Ni kwa moyo mkunjufu tunawakaribisha nyote kwenye mtandao huu.
Lengo lake ni juu ya mawasiliano ya ndovu, yakilinaganishwa na
utafiti uliofanywa na mradi wa utafiti wa ndovu wa Amboseli (Amboseli
Elephant Research Project). Mojawapo ya mbuga za wanyama maarufu
nchini Kenya, Amboseli. Wakenya watajivunia kujua kwamba habari
hii inawakilisha elimu ya muda mrefu juu ya ndovu duniani. Twajivunia
nchi hii yetu tukufu na pamoja na marafiki wa Kenya na wenzetu,
tunakusanya na kuwa shirikisha juu ya habari hii ya ndovu na sauti
zao.
Siku za usoni za wanyama wa pori na mbuga za wanyama ziko hatarini.
Kwa binadamu, maisha ya ndovu ni baathi ya vita katika taifa ambapo
mahitaji ya binadamu hutatanisha na yale ya ndovu, siku baada ya
siku. Tunatumaini kuwa mtandao huu utasaidia Wakenya kutafuta njia,
jinsi ya kuishi kwa amani na wanyama wa pori, siku za usoni. Vyema
tunavoelewa, wanyama hawa waajabu ndivyo tutakapofaidika na makabilio
na nafasinjema kwa ndovu na wanyama pori hutupa.
Tunatumaini kuwa mutapenda na kusoma yalioko kwenye mtandao huu
mara kwa mara!
|